Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramos yupo sana PSG, kuanza kukipiga hivi karibuni

Sergio Ramos 5 Sergio Ramos

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki Sergio Ramos hana mpango wa kuondoka Paris Saint Germain kwa sasa na anajiandaa na maandalizi ya kucheza mchezo wake wa kwanza ndani ya matajiri hao wa Jiji la Paris.

Ramos bado haijacheza mchezo wowote kwa PSG tangu alipojiunga kwa uhamisho huru kutoka Real Madrid, ambako alikaa kwa misimu 16.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 35, aliumia kigimbi mwishoni mwa Julai na kumfanya kuwa benchi, huku pia akikosa sehemu kubwa ya msimu wa 2020-21.

Msimu uliopita alianza katika mechi 15 za LaLiga zikiwa chache zaidi ukilinganisha na mechi 35 alizoanza msimu mwingine kabla.

Amecheza mechi tano tu kwenye mashindano yote kwa klabu hiyo mwaka 2021, sawa na dakika 395 dimbani, huku mara ya mwisho kuichezea timu ya Taifa ya Hispania ni dhidi ya Kosovo, Machi mwaka huu.

Kuumia kwa Ramos kumefanya asipate nafasi ya kuichezea timu yake mpya ya PSG na kukawa na ripoti kwamba klabu hiyo inafikiria kusitisha mkataba na mlinzi huyo wa kati.

Hata hivyo, miamba hao wa Ligue 1 walitangaza Ijumaa kwamba, Ramos anajiandaa kuanza mazoezi wiki hii na wakala wake amebainisha wazi kwamba, haondoki hapo kwenye dimba la Parc des Princes.

"Sergio atacheza haraka hivi karibuni," alisema kaka wa Ramos, Rene ambaye ni wakala wake akinukuliwa na Mundo Deportivo.

"Ataendelea kuwapo PSG na hakuna mpango wowote wa kuondoka kwa sasa, hilo halina shaka kabisa".

Chanzo: www.tanzaniaweb.live