Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramos bado hakijakaa sawa PSG, majeraha kikwazo

Sergio Ramos 2 Sergio Ramos

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sergio Ramos amerejea kwenye kikosi cha Paris Saint-Germain. Lakini hataweza kushiriki mechi ijayo.

Beki huyo wa zamani wa Real Madrid amekuwa na jeraha lililo mkwamisha msimu huu, ambayo kwa namna fulani ilichangia Los Blancos kubatilisha ofa yao ya kandarasi mpya msimu wa joto.

Staa huyu hakuweza kucheza mechi yake ya kwanza na PSG hadi wiki iliyopita, na hiyo ndiyo mechi pekee aliyocheichezea kwa klabu yake mpya hadi sasa.

Na sasa anadaiwa kuwa anenda kuikosa mechi ya PSG ya Ligue 1 dhidi ya Lens Jumamosi.

Ramos ana shida ya misuli, hii ni kwa mujibu wa kocha mkuu Mauricio Pochettino, na atakaa benchi kwa sababu hiyo.

Suala hilo linaeleweka kutokana na kurejea kwa majeruhi hivi karibuni na ukweli kwamba Ramos alicheza dakika 90 wikendi iliyopita inaweza kuchangia hali hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live