Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ramadhani Cup yamkosha Rais Karia

Wallace Kariaaaaa.jpeg Ramadhani Cup yamkosha Rais Karia

Tue, 26 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa TFF, Wallace Karia jana usiku akiwa kwenye mashindano ya Silent Ocean Ramadhan Cup amesema, TFF inayatambua mashindano ya mpira wa miguu ya ridhaa ‘amateur football’ kwakuwa tayari yamepitishwa na Kamati ya Utendaji.

“Mashindano ya aina hii [Ramadhan Cup] na mengine yanayofanana na haya tayari tumeyatambua, kikao chetu cha Kamati ya Utendaji kilipitisha kuwa tuwe na soka la amacha ukiachana na zile Ligi zetu ambazo ni professional kwa sababu sasa hivi hata mchezaji anaecheza Ligi ya Mkoa analipwa.”

“Nawapongeza Silent Ocean na Kilimanjaro Star Cago kwa kuendelea kudhamini mashindano ya Ramadhan Cup kwa mwaka wa pili mfululizo, hali ya umoja na upendo imerudi na mambo ya ugomvi hayapo. Hii inaleta maana kamili ya michezo ni umoja na upendo.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live