Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ralph Hasenhuttl akalia kuti kavu Southampton

Southampton Manager Ralph Hasenhuttl Ralph Hasenhuttl akalia kuti kavu

Mon, 7 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Southampton, Ralph Hasenhuttl amekalia kuti kavu kwani kibarua chake wakati wowote kinaweza kuota nyasi baada ya kupokea kichapo cha mabao 4-1 dhidi ya Newcastle.

Wamiliki wa klabu hiyo wameonyesha nia ya kufanya mabadiliko ya haraka iwezekanavyo kutokana na mwenendo mbovu wa timu.

Hapo awali Southampton ilitaka kusitisha mkataba na kocha huyo katika mapumziko ya Kombe la Dunia, lakini wanaweza kuchukua hatua mapema baada ya kupoteza mchezo wa jana.

Southampton watamfukuza kocha kabla ya mechi yao Ligi Kuu ya England dhidi ya Liverpool, Novemba 12 mwaka huu.

Mpaka sasa katika msimamo wa EPL, Southampton wapo nafasi ya 18, baada ya kucheza mechi 14, wakipata ushindi mechi 3, wakitoka sare mechi 3 na kupoteza mechi 8.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live