Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ralf Rangnick ampiga dongo Jesse Lingard

Ralf Rangnich Res Kocha wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa muda wa klabu ya Manchester United Ralf Rangnick amekuwa akitoa nafasi kwa wachezaji ili kuweza kumvutia tokea alipochuka mikoba ya kuinoa klabu hiyo huku akitambua kuwa kuna wachezaji wanaotaka kuondoka.

Mmoja wa wachezaji huyo ambaye hajui hatma yake kwenye klabu ya Man United ni Jesse Lingard ambaye alimshutumu kwa kuua kipaji chake baada ya kuwa na msimu mzuri kwenye klabu aliyopelekwa kwa mkopo ya West Ham, Lingard amenza kwenye mchezo mmoja tu tokea Ralf Rangnick achukue majukumu ya kuinoa klabu hiyo.

“Kwa sasa akili yangu iko kwa wachezaji wote na kuweza kuwafahamu, tumekuwa pamoja kwa takribani wiki tatu, nahisi nina wafahamu vizuri wachezaji wote tulionao kwa sasa.

“Kwangu, nahitaji kuwaendeleza wachezaji wote lakini kama mchezaji anataka kuondoka kwasababu anahisi hatapata muda wa kutosha kucheza, tunaweza kuzungumza kuhusu hilo, lakini sio kuhusu mchezaji anachotaka, ni kuhusu hali ya klabu.

“Vitu viwili ambavyo vitatuweka pamoja ikiwa mchezeji anataka kuondoka, kitu cha kwanza ikiwa anataka kuondoka, lakini kingine ni mahitaji ya klabu inabidi yatimizwe.” Alisema Ralf Rangnick

Chanzo: www.tanzaniaweb.live