Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ralf Rangnick: Manchester itegemee nini kutoka kwa kocha huyu Mjerumani?

Skysports Football Ralf Rangnick 5595178 Ralf Rangnick

Sat, 27 Nov 2021 Chanzo: BBC

Ralf Rangnick anatarajiwa kuteuliwa kuwa meneja wa muda wa Manchester United kazi ya miezi sita mpaka mwisho wa msimu huu.

Atamrithi Ole Gunnar Solskjaer, ambaye alitimuliwa katika klabu hiyo mwezi huu. Baada ya muda wake wa miezi sita kumalizika, Mjerumani huyo atachukua nafasi ya ushauri wa klabu hiyo kwa kipindi cha miaka miwili zaidi.

Lakini ni nini kiliwavutia United kwa Rangnick au nini kilichofanya Rangnick kuvutiwa na Man United? Ni meneja wa aina gani? Je, ataweza kufanikiwa na je jukumu lake baada ya msimu huu kumlizika litahusisha nini? Na je uteuzi wake utakuwa na maana gani kwa Cristiano Ronaldo?

Ili kujibu maswali haya, BBC ilizungumza na mkurugenzi wa michezo wa St. Louis SC Lutz Pfannenstiel, ambaye alifanya kazi na Rangnick huko Hoffenheim, beki wa zamani wa Leicester Christian Fuchs - ambaye alicheza chini yake katika timu ya Schalke - na waandishi wa habari wa soka wa Ulaya Raphael Honigstein, Guillem Balague na Julien Laurens.

'Mtu bora sokoni'

Uteuzi wa Rangnick unakuja baada ya kumalizika kwa mchakato wa kina uliofanywa na United, ambao walifurahishwa na Mjerumani huyo wakati wa mazungumzo ya awali mapema wiki hii.

Kocha huyo mwenye umri wa miaka 63 amejijengea sifa nzuri ya ukufunzi wakati alipokuwa Ujerumani, hasa akizifundisha timu za Stuttgart, Hannover, Hoffenheim, Schalke na RB Leipzig.

Atakuwa anajiunga na klabu ambayo iko katika nafasi ya nane kwenye Ligi kuu ya England, ikiwa imepotea chini ya Solskjaer, ambaye mechi yake ya mwisho ilikubali kipigo cha 4-1 dhidi ya Watford na ilipoteza mechi nne kati ya tano za ligi.

Honigstein: Muda si mrefu alipata ofa kama hiyo ya kazi ya kufundisha muda mfupi kutoka Chelsea akasema 'hapana, hiyo sio yangu'. Katika suala hili, kuna mambo matatu tofauti.

Kwanza, ni Manchester United na ambayo bado ni kitu bora kwake. Kuna mapenzi, haswa kwa mzungumzaji kama Rangnick, ambaye alisoma na kuishi Uingereza na anapenda Ligi Kuu.

Pili, ni miezi sita. Ni zaidi ya theluthi mbili ya msimu huu huku kukiwa na muda mrefu wa soka kuchezwa.

Tatu, United wamemwambia wazi na vyema 'tunakutaka kama meneja wa muda mfupi, lakini tunataka kwenda mbali zaidi ya kutumia ujuzi wako wa soka zaidi ya hapo'.

Pfannenstiel: Naweza kusema, Ralf ni mtaalamu mkubwa, kwa kweli ni mmoja wa makocha bora au mameneja bora Ujerumani iliyowazalishwa katika kipindi cha miaka 15-20 iliyopita.

Laurens: Ni mmoja wa watu wenye ufahamu mkubwa katika mpira wa miguu katika kipindi cha miaka 20 iliyopita na kuwapa hamasha makocha wote wakubwa Ujerumani. 'Soka lake ni la kiwango cha juu, daima inasisimu kulitazama'

Rekodi ya makombe ya Rangnick kama meneja ni ya kawaida, lakini ushawishi wake kwenye mchezo ni mkubwa, sio tu kama kocha na mkurugenzi wa kandanda lakini kama mtu mwenye akili nyingi juu ya mchezo.

Mafanikio yake makubwa yamekuwa katika kujenga timu kutoka chini kwenda juu - mfano ni vilabu vya Hoffenheim na RB Leipzig.

Anatajwa mara nyingi kama mwanzilishi wa mchezo wa kisasa unaotumiwa na makocha kama Tuchel, Julian Nagelsmann, Ralph Hasenhuttl na Jurgen Klopp, kati ya makocha ambao amewashawishi.

Pfannenstiel: Soka lake ni la moja kwa moja, anakaba sana, kasi, soka la hali ya juu - jambo ambalo huwa linasisimua kutazama.

Ukiangalia huko nyuma namna Hoffenheim ilivyokuwa inacheza, haswa jinsi RB Leipzig walivyocheza, nadhani hivi ndivyo unavyoweza kutarajia - soko la nguvu na kasi, kukabia juu na kulazimisha mpinzani kufanya makosa.

Ana falsafa ya wazi ya jinsi anavyotaka kucheza, namna anavyofunisha na soka la nguvu kukabia juu - na hilo halitabadilika kamwe.

Inatarajiwa Rangnick atachukua mikoba ya United baada ya mchezo wa Chelsea wikendi hii

United itakuwa klabu kubwa ya kwanza ya Ulaya ambayo Rangnick atakuwa ameiongoza.

Anajiunga nao baada ya usajili wa majira ya joto walipoongeza wachezaji kadhaa wa hadhi ya juu kwenye kikosi ambacho tayari kimesheheni wachezaji wa kimataifa wenye sifa kubwa, maarufu zaidi aliyejiunga ni mshindi wa Ballon d'Or mara tano Cristiano Ronaldo.

Honigstein: Daima amekuwa na mahusiano mazuri na watu , lakini watu wengine hawawezi kuwa hivyo kwa mtu anayetaka ubadilike haraka sana. Wanahisi kuudhika na kutishika, inachosha kuona mtu anayekusukuma kila wakati.

Balague: Inaonekana ni kazi ya muda na inaonekana hatari kidogo. Ikiwa unatengeneza muundo mpya, Ralf ni mtu ambaye ana wazo wazi la kile anachopaswa kufanya.

Hawezi kustahimili watu ambao hawataki kubadilika na ninahisi kuna wengi pale United. Unapaswa kuwa mzuri kwa watu na ili kusonga nao pamoja. Je, yeye ni mzuri sasa?

Honigstein: Hatakuwa na mamlaka mengi kama mtu anayekuja kwa mkataba wa miaka mitatu, lakini wakati huo huo unaweza kufanya chochote unachotaka. Anaweza kuwa mkali.

Itakuwa ngumu ikiwa Ronaldo hatakuwa kwenye mipango yake, kwa mfano. Hilo linaweza kuwa jambo moja ambalo si rahisi sana kulitatua. Ronaldo anaingiaje katika aina ya soka ya Rangnick? Labda anaweza. Labda wazo linaweza kubadilika, labda Ronaldo anaweza kubadilika? Itakuwa moja ya sehemu ya kuvutia zaidi ya simulizi hii.

Utaratibu, Muundo na mipango, siku zijazo ni mizuri'

Tangu mwaka wa 2012, Rangnick amekuwa akifanya kazi katika nafasi kadhaa za juu za ukurugenzi wa michezo, haswa akiwa na vilabu vya Red Bull hasa RB Leipzig, ambapo klabu hiyo ilipanda kutoka daraja la nne la soka la Ujerumani hadi kuwania taji la Bundesliga.

Hivi sasa ni mkuu wa michezo na maendeleo huko Lokomotiv Moscow.

Honigstein: Sina hakika kama jukumu hilo la baadaye litakuwa na nguvu halisi. Sidhani kama United wamejipanga kwa ajili hiyo.

Lakini yuko katika wakati fulani katika taaluma yake ambapo ameanzisha kampuni yake ya ushauri na anafanya kazi na vilabu, mashirikisho na wakurugenzi wa michezo.

Pfannenstiel: Tunapenda kumwita, huko Ujerumani, profesa wa mpira wa miguu. Kila kitu anachofanya kinaonekana kizuri, jinsi anavyoweka mifumo katika kila klabu ni kitu cha kushangaza.

Ukiangalia jinsi Red Bull Salzburg ilivyojengwa au jinsi RB Leipzig ilivyojengwa kutoka kituo cha mafunzo hadi timu ya kitaaluma, maendeleo ya vijana... hiyo yote ni kwa mawazo mengi na sayansi nyingi ndani yake. Utaratibu, muundo wake na mipango yake, siku zijazo unaonekana utakuwa mzuri.

Ukirejea jinsi alivyopanga kazi yake baada ya kumaliza mpango wake huko Leipzig, alitaka kuwa upande wa ushauri zaidi na ndivyo alivyofanya huko Moscow.

Kumjua Ralf na kazi yake na jinsi ulimwengu wa soka unavyofanya kazi, ikiwa atakuja na kufanya kazi ya kushangaza na kila mtu ana furaha, nadhani mpango huo wa kuwa mshauri, katika miaka miwili ijayo baada ya msimu huu, unaweza kugeuka kuwa wa muda mrefu.

Kila kitu kinawezekana na nadhani kitakuja kutokana na matokeo ya kufanikiwa kwake.

Chanzo: BBC