Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raisi wa Chama cha Soka Kenya kwenda Jela siku 14

Nick Nick Mwendwa

Mon, 15 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Raisi wa Shirikisho la mpira wa miguu nchini Kenya ashikiliwa na jeshi la polisi kwa kashfa za rushwa na atakaa rumande kwa siku 14 kupisha uchunguzi wa mashtaka hayo.

Leo jumatatu Mahakama ya nchini Kenya ilitoa kibali cha kuwaruhusu polisi kumshikillia Nick Mwendwa, raisi wa shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Kenya (FKF) kwa siku kumi na nne kupisha uchunguzi wa mashtaka ya rushwa.

Mwenda alikamatwa siku ya ijumaa baada ya Waziri wa michezo Amina Mohamed, kutangaza kusambaratika kwa shirikisho hilo baada ya serikali kufanya uchunguzi na kukuta kuna ubadhirifu wa pesa ambazo serikali ilizota na wadhamini wengine.

Mwenda mwenye miaka 41 amekuwa raisi wa shirikisho hilo tokea mwaka 2016 na amevuliwa madaraka hayo mpaka atakapothibitishwa kuwa hana hatia, na kwa sasa Waziri ametangaza baraza ambalo litaongoza taasisi hiyo kwa muda wa miezi sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live