Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Zamalek atupwa jela kwa kumtusi Rais wa Al Ahly

Mortada Mansour Zamalek .jpeg Mortada (kulia) na Mahmoud (kushoto)

Tue, 28 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zamalek, Mortada Mansour amehukumiwa kifungo cha mwezi mmoja jela katika kesi aliyoshtakiwa na Rais wa Al Ahly, Mahmoud al-Khatib.

Mansour, ambaye ni Mbunge wa zamani alikuwa akitumia nafasi yake hiyo kuzuia kushtakiwa lakini baada ya kupoteza katika uchaguzi wa Mwaka 2020 akafunguliwa mashtaka na kuhukumiwa kifungo cha Mwaka mmoja lakini alikata rufaa na kifungo chake kupunguzwa.

Kwa Sheria ya Misri akitoka jela hataweza kuendelea na nafasi yake ya kuiongoza Zamalek kutokana na aina ya hukumu aliyokutana nayo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live