Rais wa klabu ya Zamalek ya Misri, Mortada Mansour ameonyeshwa kukasirishwa na kitendo cha mashabiki wa timu hiyo waliovalia nguo nyeusi na kutengeneza umbo la sura yenye hasira wakati timu yao ikicheza dhidi ya Al-Merreikh ya Sudan.
Katika mechi hiyo licha ya Zamalek kushinda mabao 4-3 hayakusaidia kuivusha timu hiyo hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika wakishika nafasi ya 3 kitendo kilichotafsiriwa kuwa mashabiki hao hawakuridhishwa nacho.
"Zamalek huwa tunavaa jezi nyeupe yenye mistari mekundu mwili kwa anayetaka kuja kutushangilia anakaribishwa ila sio kuvaa nyeusi" amesema Rais Mansour na kuongeza;
"Wale waliokuja kwenye mechi na nguo nyeusi hawataruhusiwa kuingia kwenye mechi tena."