Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Wydad awatangazia 'kiama' Simba SC

Rais Wa Wydad Awatangazia Kiama Simba SC Rais wa Wydad awatangazia 'kiama' Simba SC

Tue, 5 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa klabu ya Wydad AC, Said Naciri jana wakati anahojiwa na chombo cha habari LE Matin alisema amewajibika kwa matokeo mabaya ya timu.

“Nimewajibika kwa matokeo mabaya ya Timu yangu na nimefanya kikao na benchi la ufundi pamoja na wachezaji ili kutatua changamoto hii, nilikuwa sihudhurii mechi za timu yangu ila hivi sasa nitafanya vya kutosha na timu yetu itafanya vizuri mechi zijazo.”

Wydad imecheza michezo miwili hadi sasa kwenye kundi B na kuambulia vipigo mechi zote, kunaifanya timu hiyo ishike mkia kwenye msimamo wa kundi hilo likiwa linaongozwa na ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Mechi ifuatayo kwa Wydad AC ni dhidi ya Simba SC itakayopigwa nchini Morocco siku ya Jumamosi Disemba 9,2023 mida ya saa 4:00 usiku.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live