Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Uganda (FUFA) Moses Magogo, ameeleza ni kwa nini Ligi Kuu ya Tanzania NBC imepiga hatua kubwa hadi kuwa na ushindani katika miaka kadhaa iliyopita huku ligi za Kenya na Uganda zikiwa zimedorora,
Mnamo mwaka wa 2023, Ligi Kuu ya Tanzania ilitajwa kuwa ligi ya tano kwa kwa ubora barani Afrika na ya 38 kwa ubora duniani katika takwimu zilizotolewa na Shirika la Kimataifa la Historia ya Soka na Takwimu (IFFHS).
Ufichuzi huo ulikuwa kiashirio cha jinsi gani ligi ya Tanzania ilivyopanda, huku takwimu zikisema ni jinsi gani ligi za kandanda za Uganda na Kenya zilivyorudi nyuma
Tanzania ilipata mtaji mkubwa wa kuitangaza na kuikuza ligi hiyo kupitia klabu kubwa za Yanga Sc na Simba Sc katika michuano ya kimataifa ya Caf.
Ndani ya miaka mitano klabu ya Simba SC imefanikiwa kucheza hatua ya robo fainali ya Klabu Bingwa Afrika mara 3 na robo fainali moja ya Kombe la shirikisho Afrika, huku Yanga Sc akicheza fainali moja ya Kombe la shirikisho Afrika msimu uliopita.