Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Ghana aipongeza timu yao ya Taifa

Rais Wa Ghana Aipongeza Timu Yao Ya Taifa Rais wa Ghana aipongeza timu yao ya Taifa

Fri, 25 Nov 2022 Chanzo: Bbc

Rais wa Ghana Nana Akufo-Addo amesifu "uchezaji wa kishindo" wa timu ya taifa katika mchezo wao wa kwanza wa Kombe la Dunia dhidi ya Ureno ambao uliisha kwa mabao 3-2.

Black Stars imekuwa timu ya kwanza ya Kiafrika kufunga bao katika michuano ya mwaka huu, lakini iko mkiani mwa Kundi H.

Itacheza na Korea Kusini tena Novemba 28.

Katika ujumbe wake wa Twitter, Rais Addo alisema "anajivunia timu nzima" licha ya kupoteza dhidi ya Ureno.

Aliongeza: "Wana nafasi ya kupigana tena siku nyingine na wameonyesha wanachohitaji kufanya ili kukabiliana na timu yoyote kwenye mashindano."

Chanzo: Bbc