Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa FIFA aipongeza Simba SC

Infantino Gianni FIFA Rais wa FIFA aipongeza Simba SC

Tue, 9 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Duniani (FIFA), Gianni Infantino ametuma salamu za pongezi kwa Mabingwa wa Ligi Kuu ya Wanawake (TWPL) 2023/2024 timu ya Wanawake ya klabu ya Simba, Simba Queens.

Taarifa ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) imeeleza kuwa Infantino amesema juhudi za Simba Queens za msimu mzima zimezaa matunda na kufanikisha kupata taji hilo. huku akiwapongeza wanachama wote wa Klabu hiyo kwa mafanikio hayo.

Aidha Infantino amemshukuru Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kwa kazi nzuri na kujitolea kwa maendeleo ya mpira wa miguu wa wanawake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live