Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais wa Barcelona Kortini kwa Rushwa

Joan Laporta Bn Rais wa Barcelona, Joan Laporta

Thu, 19 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta ameshtakiwa na Mahakama Nchini Uhispania kwa tuhuma za rushwa. Barcelona inatuhumiwa kwa kumlipa aliyekuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Kiufundi ya Waamuzi, Jose Maria Enriquez Negreira zaidi ya euro milioni 7.3 kati ya mwaka 2001 na 2018.

Jaji anayesimamia kesi hiyo inayojulikana kama 'Caso Negreira' huko Uhispania ameamua kumfungulia mashtaka Rais Laporta kwa rushwa, ufisadi kwenye michezo, utawala usio wa haki na kughushi.

Caso Negreira' inahusisha malipo ya jumla ya takriban dola milioni 7.7 (€7.3 milioni) ambayo Barca walilipa kwa Negreira na mwanawe kwa kipindi cha miaka 18 kinachochunguzwa.

Hata hivyo Laporta amekanusha mara kadhaa kwamba Barca hawafanya makosa yoyote na kusisitiza kuwa malipo hayo yalifanywa kwa kuwa Negreira alifanya kazi yake kwa uaminifu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live