Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais soka Zanzibar atoa neno uchaguzi TFF

Rais Soka Pic Data Rais soka Zanzibar atoa neno uchaguzi TFF

Sat, 7 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Rais wa Chama cha Soka visiwani Zanzibar (ZFA), Abdulratif Yassin amewapa neno wapiga kura kwenye uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) unaokwenda kufanyika saa chache zijazo kwenye hoteli ya Tanga Beach Resort mjini Tanga.

Abdulratif ni miongoni mwa waalikwa kwenye uchaguzi huo uliotanguliwa na mkutano mkuu wa TFF.

Baada ya kupewa nafasi ya kuzungumza, mwenyekiti huyo wa ZFA amewataka viongozi watakaochaguliwa kulitendea haki soka la Tanzania.

"Mnakwenda kuchagua safu itakayoboresha soka, hiki mnachokifanya hapa ni kwa ajili ya wengi na kulitendea haki soka la Tanzania," amesema.

Mbali na kiongozi huyo, mwakilishi wa Shirikisho ka Soka la kimataifa (Fifa), Solomon Mdege ametaka uchaguzi huo uwe huru na wa haki.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz