Rais wa Gasogi United ya Rwanda, Kakooza Nkuriza Charles ametangaza kuiondoa klabu hiyo katika mashindano yote kwa madai ya dhuluma zinazofanywa ndani ya soka nchini humo.
Kakooza amechukua uamuzi huo baada ya kufungwa bao 1-0 na AS Kigali katika mashindano ya Ligi Kuu Rwanda kwenye uwanja wa Kigali Pele maeneo ya Nyamirambo Jumamosi hii.
Rais huyo amewanyoshea kidole waamuzi kuwa chanzo cha kudorora kwa michezo iwe ni kwa upande wa ligi kuu, timu za vijana na Nyanja nyingine za michezo.
Amesema kuwa anakwenda kuwalipa wachezaji wote wanaoidai klabu ili waruhusiwe kwenda kutafuta kwingine wanapohitaji.