Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Yanga atoa tamko kibarua cha Nabi

Nabi X Injinia Hersi.jpeg Injinia Hersi na Nabi

Tue, 11 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati uvumi ukizagaa kwamba uongozi wa Yanga haufurahishwi na mwenendo wa timu yao hasa baada ya kutoa sare nyumbani dhidi ya Al Hilal, Rais wa klabu hiyo injinia Hersi Said amekanusha taarifa hizo.

Hersi akizungumza na kituo cha radio cha E fm kupitia kipindi cha michezo amesema uongozi wake wala haujampa mechi kocha wao huyo.

Hersi amesema Yanga inaendelea kujiandaa na mechi ya marudiano dhidi ya Wasudan hao kusaka tiketi ya kucheza hatua ya Makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika huku kocha wao akiwa Nabi.

"Kocha Nabi hajapewa mechi moja wala mbili, bado ni mwalimu wetu, hatufanyi kazi kwa mihemko ya watu, yuko pale kama kocha wetu mkuu na ameijenga timu yetu,"amesema Hersi.

"Tumepata msaada mkubwa kutoka kwa Balosi wa Tanzania kule Khartoum, mashindano ya Afrika yamekuwa na mazingira magumu haswa ugenini lakini tumejiandaa na tumepunguza idadi ya siku za kukaa kule ili kupunguza hizo hujuma."

Aidha Hersi amesema Yanga iko makini kuekekea mechi hiyo huku akijivuniua uzoefu wa wachezaji wao katika mazingora ya kucheza ugenini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live