Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Yanga aalikwa Tuzo za COSAFA

Injinia Hersi COSAFA Rais Yanga aalikwa Tuzo za COSAFA

Fri, 10 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Yanga SC, Hersi Said @caamil_88 amealikwa na Chama cha Soka Ukanda wa Kusini (COSAFA) nchini Afrika Kusini na kutoa tuzo kwa mchezaji wa taifa hilo, Janine Van Wyr.

Hersi alihudhuria katika tuzo hizo zilizofanyika katika Jiji la Johannesburg na kutoa tuzo ya LIFE TIME ACHIEVMENT kwa nyota huyo wa Soka la Wanawake.

Rais huyo wa @yangasc alifurahi kualikwa katika tuzo hizo za COSAFA AWARDS 2023 na kuandika kuwa “ Imekuwa ni heshima kubwa kwangu kualikwa na kupata nafasi ya kukabidhi tuzo ya LIFE TIME ACHIEVEMENT kwa LEGENDARY wa soka la wanawake katika ukanda wa kusini mwa afrika, COSAFA ikienda kwa JANINE van WYR.

“ Mwanasoka huyu JANINE van WYR, mwenye rekodi ya kucheza mechi nyingi zaidi barani Afrika akiwa na BANYANA BANYANA kwa zaidi ya miaka 19 (185 matches) akimzidi nguli wa soka la kiume AHMED HASSAN wa EGYPT huku akiwa nahodha kwa zaidi ya miaka 10, amekuwa na mchango mkubwa kwenye soka la wanawake hata baada ya kustaafu kwa kuanzisha timu ya vijana.

Leo, mchango wake huu unatambuliwa rasmi na COSAFA na kupitia TUZO hizi, kwa heshima na taadhima nimepewa nafasi hii adhimu ya kukabidhi nishani ya COSAFA LIFETIME ACHIEVEMENT AWARD 2023 kwa mwanadada JANINE van WYR.

“ Pongezi kwako legendary wa soka la wanawake barani Afrika, JANINE van WYR “ aliandika Hersi

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: