Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Yanga: Tunaleta Kombe la CAF nyumbani

Hersi Said 1.png Rais wa Klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said

Thu, 16 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati Yanga wakijiandaa kuwavaa US Monastir siku ya Jumapili Machi 19, mchezo wa mzunguko wa tano hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Afrika.

Tayari Uongozi wa Klabu hiyo umeshapiga mahesabau namna ya kulibeba kombe hilo na kulishusha mitaa ya Jangwani.

Akizungumza Rais wa Yanga injinia Hersi Said amesema;

"Sisi Yanga SC ndio tutakuwa timu ya kwanza kutoka kwenye ardhi ya Tanzania kulileta Kombe la CAF nchini Inshallah, Jumapili tukifanikiwa kutinga Robo fainali nina imani tutavuka na kwenda Nusu fainali , baadae Fainali na Inshallah sisi ndio itakuwa timu ya Kwanza kushangilia taji hili"

"Wananchi msiwe na hofu Inshallah sisi mwaka huu tutalibeba"

Yanga wanakamata nafasi ya pili katika msimamo wa kundi D wakiwa na alama 7 wakihitaji alama tatu kufuzu kwa hatua ya Robo Fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live