Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Yanga: Nina imani kubwa na Morisson

Hersi Said Vs Morisson Rais wa Yanga Injinia Hersi Said bado anaamini uwezo wa winga Bernard Morisson klabuni hapo

Mon, 20 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kama ulidhani Bernard Morrison ana mgogoro na klabu yake ya Yanga basi sahau, baada ya ripoti nyingi kuwa Morrison aliondoka nchini kwenda kwao Ghana kwa matatizo ya kifamilia kwa mujibu wa Afisa Habari wa Timu hiyo Ali Kamwe.

Hatimaye Rais wa Klabu ya Yanga Eng. Hersi Said alisema kuwaana imani kubwa na na Bernard Morrison.

“Nina imani kubwa na Bernad Morrison. Yupo katika matibabu na kama klabu tutahakikisha anarejea uwanjani akiwa mwenye afya njema ili aendelee kuitumikia timu yetu. “ Eng. Hersi Said Rais wa Yanga SC .

Bernard alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha kubwa msimu wa 2022/23, akitokea kwa watani zao Simba SC, lakini kabla ya hapo alitokea Yanga ikiwa ni klabu yake ya kwanza kumtambulisha hapa nchini ambapo alicheza kwa nusu msimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live