Rais wa shirikisho la soka barani Ulaya, Aleksander Ceferin, ametupilia mbali tetesi zinazoendelea katika mitandao ya kijamii juu ya uwezekano wa vilabu vya ligi ya saudia kushiriki michuano ya klabu bingwa ulaya (UEFA)
Rais huyo alisema kuwa "Ni vilabu kutoka bara la Ulaya pekee, ndio vinaweza kushiriki Ligi ya Mabingwa, Ligi ya Europa na Ligi ya Conference."
"Vyombo vya habari vilitoa taarifa hizi bila hata kutuuliza," aliongeza Ceferin.
Akizungumza kuhusu maendeleo ya soka, hasa kuibuka kwa ligi ya Saudi Arabia, Rais Ceferin alilinganisha ligi ya Saudi Arabia na ligi ya China, ambayo miaka michache iliyopita pia ilivutia nyota kadhaa.
"Saudia si tishio, China walitumia mbinu sawa na hizo, soka la China halikuendelea na hawakufuzu kwenye Kombe la Dunia."
"Hiyo si njia sahihi, Wanapaswa kufanyia kazi maendeleo ya wachezaji wachanga na makocha, lakini hilo si tatizo langu."
Ceferin alisisitiza kuwa wachezaji walio kwenye kiwango bora kama Haaland na Mbappe hawana ndoto ya kucheza huko, na Saudi Arabia si mshindani wa Ulaya.