Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia kununua goli sh Mil 5 mechi za Kimataifa Simba, Yanga

Rais Samia Aridhia Wanafunzi 28,000 Kwenda Vyuoni Rais Samia kununua goli sh Mil 5 mechi za Kimataifa Simba, Yanga

Tue, 14 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu ametangaza kulinunua kwa Tsh. Milioni 5 kila goli litakalofungwa na Simba au Yanga katika michezo yao inayochezwa weekend hii wakiiwakilisha Tanzania kwenye Michuano ya Shirikisho.

Taarifa hiyo imetolewa kwa Wahariri na Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa leo Dar es salaam ambapo amenukuliwa akisema “Rais Samia amenituma nisemae kila goli litakalofungwa na Yanga au Simba ametangaza kulinunua kwa Tsh. Milioni 5”

“Kazi kwenu Wachezaji ukifunga magoli mawili una Tsh. Milioni 10, ukifunga magoli matano una Tsh Milioni 50, lengo lake pamoja na kufunga magoli Timu zetu lazima zishinde kwenye michuano hii”

Simba SC ni Wawakilishi wa Tanzania katika michuno ya Club Bingwa Afrika na watacheza dhidi ya Raja Casablanca ya Morocco Jumamosi hii uwanja wa Mkapa wakihitaji ushindi ili kujiweka pazuri katika Kundi wakati Yanga SC wenyewe wanacheza Jumapili kwa Mkapa dhidi ya TP Mazembe ya Congo DR katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika wote wanahitaji ushindi ili kumaliza nafasi mbili za juu na baadae kukata tiketi ya robo fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live