Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia awapongeza Simba kuwakanda Yanga

Rais Samia Awapongeza Simba Kuwakanda Yanga Rais Samia awapongeza Simba kuwakanda Yanga

Mon, 17 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amewapongeza klabu ya Simba SC kwa kuibuka na ushindi katika mechi dhidi ya wapinzani wao wa jadi, Yanga SC.

Simba iliibuka na ushindi wa goli 2-0 jana katika mechi hiyo ya Ligi Kuu iliyopigwa katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar ambapo magoli hayo yaliwekwa kambani na beki Henock Inonga na Kibu Denis.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rais Samia aliweka ujumbe huo.

"Hongereni Simba kwa ushindi wenu dhidi ya Yanga katika mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara. Upinzani wenu wa jadi uwanjani ni burudani inayowaleta pamoja mamilioni ya Watanzania katika kila kona ya nchi yetu, kwa namna ya kipekee. #KariakooDerby."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live