Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia awapongeza Simba kutinga makundi Klabu Bingwa

Simba Kikosi Cha Kwanza Rais Samia awapongeza Simba kutinga makundi Klabu Bingwa

Mon, 17 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan, amewapongeza Simba SC kwa kufanikiwa kutinga hatua ya Makundi ya Klabu Bingwa Afrika.

Simba ilitinga hatua hiyo jana Oktoba 16, 2022 katika Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar baada ya kuwafunga goli moja kwa bila vijana wa Agosto kutoka Angola.

Kupitia ukuara wake wa Instagram ambao upo varrified, Rais Samia aliposti picha ya kikosi cha Simba na kusindikiza na ujumbe wake wa pongezi.

"Kongole @SimbaSCTanzania kwa ushindi wa 1-0 (ushindi wa jumla 4-1) mlioupata dhidi ya timu ya Primeiro De Agosto ya Angola na hivyo kufanikiwa kuingia hatua ya makundi ya klabu bingwa Barani Afrika. Nawatakia kila kheri katika michuano inayofuata."

Katika mchezo wa awali uliopigwa nchini Angola, Simba aliafinikiwa kuwapiga Agosto goli 3-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live