Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia awapongeza Simba, Yanga

RAIS SAMIA SIMBA YANGA Rais Samia awapongeza Simba, Yanga

Mon, 24 Apr 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, amevipongeza vilabu vya Simba SC na Yanga SC kwa ushindi walioupata kwenye mashindano ya Kimataifa.

Simba SC ilimtandika Wydad Casablanca 1-0 Jumamosi Aprili 22, 2023 kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar ikiwa ni mechi ya kwanza ya Robo Fainali ya Klabu Bingwa Afrika huku Yanga jana ikimkanda Rivers United 2-0 mchezo wa kwanza wa Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika uliopigwa nchini Nigeria.

Baada ya ushindi huo, Rais Samia alindika kwenye mitandao yake ya kijamii, Instagram pamoja na Twitter:

"Hongereni watani wa jadi Simba na Yanga kwa ushindi katika michezo yenu ya CAF (Klabu Bingwa Afrika na Kombe la Shirikisho) wikiendi hii. Ahadi ya hamasa kwa kila goli bado iko pale pale. Endeleeni kutuwakilisha vyema. Nawatakia kheri."

Chanzo: www.tanzaniaweb.live