Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia aitaka Simba ijipange msimu ujao

#LIVE: Rais Samia Anahutubia Mbele Ya Rais Wa Ujerumani Rais Samia aitaka Simba ijipange msimu ujao

Sat, 6 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan ameitaka Simba ijipange kwaajili ya msimu ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kutolewa kwenye robo fainali ya michuano hiyo na bingwa mtetezi Al Ahly leo kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Cairo, Misri

Rais Samia ameandika kwenye mitandao yake ya kijamii “chezo mzuri Simba. Usiku haukuwa wa ushindi lakini tumeziona juhudi na zinatupa faraja na matarajio kuwa, msimu ujao wa mashindano ya Ligi ya Mabingwa ya Shirikisho la Soka Afrika mambo yatakuwa mazuri zaidi. Ahadi yetu ni kuendelea kuwaunga mkono na kuwapa motisha.”

Simba imeishia Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara ya nne katika misimu sita baada ya kupokea kichapo cha jumla ya mabao 3-0 na Al Ahly bingwa mtetezi wa michuano hiyo.

Simba imepoteza ugenini mabao 2-0 Cairo yakifungwa Amr El Solia dakika ya 47 na Mahmoud Kahraba kwa penalti dakika ya 90 huku bao la kwanza lilifungwa na Ahmed Nabil Koka Machi 29, katika Uwanja wa Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live