Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia aipongeza Serengeti Girls

Rais Samia 1024x640 Rais Samia Suluhu Hassan

Wed, 19 Oct 2022 Chanzo: dar24.com

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameipongeza Timu ya Taifa Tanzania ya Wanawake chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti Girls’, baada ya kufuzu hatua ya Robo Fainali Kombe la Dunia.

Serengeti Girls imetinga hatua hiyo, kufuatia matokeo ya sare ya 1-1 dhidi ya Canada ilioyapata jana Jumanne (Oktoba 18) nchini India zinapoendelea Fainali hizo.

Rais Samia ametoa pongezi hizo kupitia Ukurasa wake wa Mtandao wa Kijamii wa Instagram, huku akiitakia timu hiyo kila la kheri katika mchezo wa Robo Fainali ambao watacheza dhidi ya Colombia, Jumamosi (Oktoba 22).

Rais Samia ameandika: Mmenifurahisha sana Watoto wangu @serengetigirls kwa kuandika historia ya kufuzu kuingia robo fainali ya Michuano ya Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya miaka 17 nchini India. Mmefanya jambo kubwa kwa nchi yetu Tanzania na nawatakia kheri katika hatua ya robo fainali.

Serengeti Girls iliweka matumaini ya kufuzu Robo Fainali, baada ya ushindi dhidi ya Ufaransa siku ya Jumamosi (Oktoba 15), hivyo matokeo ya sare dhidi ya Canada na Japan kushinda dhidi ya Ufaransa yaliivusha timu hiyo ya Tanzania.

Colombia inakutana na Serengeti Girls, baada ya kuongoza Kundi C ikiwa na alama sita sawa na Mabingwa watetezi Hispania iliyozidiwa uwiyano wa mabao ya kufunga na kufungwa.

Michezo mingine ya Robo Fainali Kombe la Dunia kwa Wanawake chini ya umri wa miaka 17, itashuhudia Marekani ikicheza dhidi ya Nigeria Oktoba 21 katika Uwanja wa DY Patil mjini Mumbai, huku siku hiyo hiyo Ujerumani itaikabili Brazil.

Kikosi cha Japan kitacheza dhidi ya Mabingwa watetezi Hispania Oktoba 22 katika Uwanja wa Pandit Jawaharlal Nehru mjini Margao, ambao pia utashuhudia Tanzania ikipapatuana na Colombia siku hiyo.

Chanzo: dar24.com