Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Samia: Ninafuatilia sana Ndondo Cup

Samia Road.jpeg Rais Samia

Tue, 6 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais Samia Suluhu Hassan, jana usiku Ikulu Jijini Dar es salaam wakati wa chakula cha jioni kuipongeza Yanga, ameweka wazi kuwa yeye ni Mfuatiliaji mkubwa wa Mashindano ya soka ya Ndondo Cup pamoja na Yamleyamle ya Zanzibar ambayo huibua vipaji vya soka kutoka mtaani na kuvipa nafasi ya kuonesha uwezo.

“Nikiwa Mama mlezi wa Vijana Tanzania katika fani mbalimbali nina dhima ya kulea na kukuza vipaji, nimekuwa nikifuatilia sana mashindano yanayofanyika ngazi za chini nimekuwa nikifuatilia sana Ndondo Cup pia Yamleyamle kule Zanzibar”

“Ni mashindano yanayovuta Watu wengi pia yanakuza vipaji kuja kulisha Timu kubwa, nataka niwaambie nipo pamoja nanyi na nitaangalia namna ya kuwashika mkono ili muendelee kusonga mbele”

Ndondo Cup ni Mashindano ambayo huandaliwa chini ya Clouds Media Group @CloudsMediaLive chini ya usimamizi wa kitengo chake cha michezo kikiongozwa na Shaffih Dauda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live