Rais Samia Suluhu Hassan jana June 05,2023 kwenye chakula cha jioni alichowaandalia Yanga kuwapongeza kwa hatua waliyofikia ya kucheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF) amemuomba Mfanyabiashara na Mdhamini wa Yanga SC, Ghalib Said Mohamed (GSM) kuendelea kusaidia michezo na kwamba yeye na Wafanyabiashara wengine hawabinywi na Serikali bali wamepewa nafasi nzuri ya kufanya biashara.
“Natoa wito kwa Wadau kusaidia michezo kwani uendeshaji wa michezo una gharama kubwa, hapa namuona Ghalib (GSM) akijua kuna mashindano mbele flesh ya nyama inapungua kidogo anapiga mahesabu zitanitoka ngapi lakini zikutoke tu Baba yangu ndilo eneo ulilochagua na ndilo eneo Mungu alilokupangia kwa hiyo zitoe”
“Na kwa bahati nzuri Mimi wala sikubinyi kabisa nimekupa nafasi fanya biashara, wewe na wenzio hambinywi kabisa kwahiyo zile ambazo sisi hatubinyi pelekeni kwenye michezo”