Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais PSG amjibu Lionel Messi

Messi X PSG Prezidaaa Rais PSG amjibu Lionel Messi

Wed, 27 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa PSG Nasser Al-Khelaifi amemjibu Lionel Messi kufuatia madai kuwa klabu hiyo haikufanya chochote kusherehekea mafanikio ya Argentina Kombe la Dunia.

Baada ya kurejea Ufaransa,Argentina wakiwa mabingwa wa kombe la Dunia 2022 , Messi alihisi kuwa ndiye mchezaji pekee ambaye 'hakutambulika katika klabu yake', huku nyota kama Lisandro Martinez na Alexis Mac Allister waliopongezwa na Klabu zao.

Rais wa PSG Al-Khelaifi amekanusha madai hayo kwenye mahojiano na RMC Sports kwamba mafanikio ya Messi hayakupongezwa baada ya kurejea kwake, akisema kuwa Argentina walikuwa wametoka kuifunga Ufaransa kwenye fainali ingekuwa ngumu wao kama Klabu ya Ufaransa kufurahi hadharani.

“Kama kila mtu aliona, kwa sababu hata tulipost video, tulimsherehekea Messi kwenye mazoezi, na hata nyuma ya pazia,"

"Lakini kwa heshima, sisi ni klabu ya Ufaransa ilikuwa ngumu kusherehekea uwanjani ni lazima tuheshimu nchi, wachezaji wenzake kwenye timu yetu"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live