Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Mwinyi akutana na Rais wa CAF

Rais Mwinyi Akutana Na Rais Wa CAF Rais Mwinyi akutana na Rais wa CAF

Fri, 24 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi ameushukuru uongozi wa Shirikisho la Soka Afrika(CAF) kwa kuifanya Zanzibar kuwa mmoja ya waandaaji wa Mashindano ya African Football Championship mwaka huu.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipokutana na Rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF), Dk.Patrice Motsepe na ujumbe wake waliofika Ikulu Zanzibar tarehe: 24 Mei 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amesema Zanzibar itaendeleza na kudumisha uhusiano wake na CAF .

Rais Dk.Mwinyi amemueleza Dk.Motsepe kuwa Zanzibar inahitaji msaada wa kuendeleza vipaji vya soka kuanzia ngazi za academy kwa kushirikiana na CAF.

Rais wa CAF Dk.Motsepe leo atashuhudia mchezo wa kwanza wa fainali za Mashindano ya African Schools Football Championship yanayofanyika katika uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live