Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Marcelo avunja Bunge la Ureno

Marcelo Rebelo De Sousa Marcelo Rebelo de Sousa.

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Ureno, Marcelo Rebelo de Sousa amelivunja bunge la taifa hilo na kuitisha uchaguzi wa mapema, ikiwa ni siku mbili baada ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Antonio Costa kujiuzulu na serikali yake kwa kashfa za rushwa.

Katika hotuba yake aliyoitoa kwa Umma kupitia televisheni ya taifa baada ya kukutana na Baraza la Taifa linalohusisha wanasiasa wa zamani na waliowahi kuwa watu mashuhuri na baada ya mkutano na viongozi wa vyama vilivyoko bungeni hapo jana Rebelo de Sousa amesema uchaguzi mpya huenda ukafanyika Machi 10 mwakani 2024.

Waziri mkuu Antonio Costa aliiongoza Ureno tangu mwaka 2015, na kushinda kwa kishindo kwenye uchguzi wa Julai mwaka uliopita.

Alijiuzulu mara moja kufuatia msako mkali wa polisi siku ya Jumanne, kama sehemu ya uchunguzi wa tuhuma za rushwa ambapo mkuu wake wa utumishi pamoja na watu wengine wanne walikamatwa, huku waziri mmoja akitajwa kama mtuhumiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live