Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Macron awatumia ujumbe Real Madrid sakata la Mbappe

Yswfdywdywd Rais Macron awatumia ujumbe Real Madrid sakata la Mbappe

Wed, 8 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa 25 wa Ufaransa Emmanuel Macron amemtumia ujumbe wa wazi nyota wa klabu ya PSG Kylian Mbappe pamoja na klabu yake mpya [Real Madrid] atakayojiunga baada ya kumaliza mkataba wake na PSG akiitaka klabu hiyo imuachie acheze michuano ya Olympic.

"Nina imani kuwa klabu zote za Ulaya zitawaachia wachezaji wake kama ambavyo klabu za Ufaransa zitafanya na hiyo ndio roho ya Michuano ya Olympic".

"Nilikutana na Baba yake Mbappe wiki iliyopita na nilimuuliza swali akaniambia 'Anataka kucheza Olympics'".

- Amesema Emmanuel Macron, Rais wa Ufaransa.

Mbappe awali aliwahi kusema kuwa hatashiriki michuano ya Olympic.

"Maamuzi yangu hayajabadilika, lakini ukweli ni kuwa sifikirii kuhusu Olympic, najali zaidi kuhusu sasa hivi na sasa ni kuhusu PSG."

- Kylian Mbappe, Nyota wa klabu ya PSG.

Real Madrid imetoa waraka wazi kuwa haitawaachia wachezaji wake kwenda kushiriki michuano ya Olympic ikiwa pia Mbappe anatarajiwa kujiunga na klabu hiyo July 1 mwaka huu.

Real Madrid itashuka dimbani leo kuikabili Bayern Munich majira ya saa nne [22:00] usiku kwenye mchezo wa nusu fainali ya Ligi ya mabingwa Barani Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live