Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Karia azipongeza Simba, Yanga

Wallace Karia Bila Vijana Rais Karia azipongeza Simba, Yanga

Mon, 4 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amezipongeza Klabu za Young Africans na Simba SC kwa kufuzu hatua ya robo fainali Ligi ya Mabingwa Afrika (CAFCL).

Katika salamu zake za pongezi, Karia amesema kwa timu mbili za Tanzania kufika hatua ya robo fainali CAFCL ni kielelezo cha kukuwa kwa mpira wa miguu wa Tanzania ambao umekuwa ukipiga hatua kusogea mbele.

Rais Karia amesema uwekezaji mkubwa unaofanywa na wadau mbalimbali umekuwa chachu kubwa ya maendeleo ya mpira wa miguu nchini kiasi cha kufanya vizuri katika mashindano mbalimbali yakiwemo ya CAFCL.

Ameziomba Klabu za Simba SC na Young Africans kuhakikisha zinaendelea kujiandaa vizuri na kufanya vizuri katika michezo ya hatua inayofuata.

Aidha amewapongeza wadau mbalimbali wa mpira wa miguu ambao wamekuwa sehemu ya mafanikio hayo.

Hii ni mara ya kwanza kwa Tanzania kupeleka timu mbili katika hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya CAF.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live