Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais Karia awashukia Wachambuzi nchini

Rais Karia Rais wa Shirikisho la Soka Nchini Tanzania, Wallace Karia

Thu, 3 Mar 2022 Chanzo: eatv.tv

Akizungumza na Kipenga cha East Africa Radio, Rais wa TFF, Wallace Karia amesema wametoa miezi miwili kuruhusu mjadala hadi kwa Waandishi wa Habari kupata maoni pia ili kuboresha zaidi lakini ameongeza kuwa kupitia kamati ya utendaji wamewasilisha mpango huo na utekelezaji uanze haraka.

''Tuna document tumeiwasilisha kwenye kamati ya utendaji, tumeamua kuchokoza, tumetoa miezi miwili kuruhusu mjadala hata kwa Waandishi wa Habari, tunataka Ligi za Mikoa na Wilaya ichezwe na wachezaji wenye umri usiozidi miaka 20, lengo ni kuwapa jukwaa kubwa vijana kucheza na kuonyesha vipaji vyao'' amesema Rais karia.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa ufunguzi wa kozi ya FIFA Grassroot kwa makocha kutoka mikoa mbalimbali nchini itakayofanyika kwa siku tano huku akifurahishwa na mwamko wa waashiriki waliojitokeza kwa wingi huku akiguswa zaidi na uwepo wa Waandishi wa Habari.

"Nimefurahi kuwaona wanahabari na Wachambuzi kuja kusoma kozi hii ya ukocha, maana kuna watu wanajiita wachambuzi sijui wamesomea wapi uchambuzi"

"Hawa ambao watu wanajiita Wachambuzi hawautendei haki mpira wetu, wanasikilizwa na watu alafu wanatoa maoni yao binafsi ya ushabiki wao, jambo hili mara nyingi nalitazama na kuona kuwa wao wanapotosha na kuleta taharuki na chuki"

"Sisi tumebarikiwa kuwa na timu za Simba na Yanga, wenzetu hawajabarikiwa kuwa nazo lakini tunazitumia vibaya kwa chuki, ubinafsi kiasi ambacho imekuwa hatari zaidi kwenye Soka letu"

Chanzo: eatv.tv