Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais FC Barcelona ajitoa muhanga

Barca Ms.png Rais FC Barcelona ajitoa muhanga

Tue, 12 Dec 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Rais wa Klkabu Bingwa nchini Hispania FC Barcelona, Joan Laporta amepanga kukutana na kufanya mazungumzo na wawakilishi wa Mshambuliaji wa Atletico Madrid anayecheza kwa mkopo kwenye kikosi chao, Joao Felix na kiungo, Joao Cancelo ambaye pia anacheza kwa mkopo akitokea Manchester City.

Mastaa hao ambao wote wanatokea Ureno wameonyesha viwango vya kuvutia na Barca imepanga kuwasajili jumla ama kuwachukua tena kwa mkopo kuelekea msimu ujao.

Taarifa za awali zinaeleza Atletico Madrid inahitaji kiasi kisichopungua Pauni 60 hadi 68 Milioni ili kumpiga bei Felix wakati Man City ikihitaji Pauni 44 Milioni kumwachia Joao Cancelo.

Hata hivyo maboasi Barca wanaona pesa hizo ni nyingi hivyo wamepanga kuzishawishi pande zote kuhakikisha wanapunguza bei ili waweze kukamilisha dili hizo katika dirisha lijalo la usajili au mwishoni mwa msimu.

Tangu atue Barca, Felix mwenye umri wa miaka 24 ambaye mkataba wake na Atletico unamalizika mwaka 2029, amefunga mabao matano kwenye mechi 17 za michuano yote alizocheza wakati Cancelo mwenye umri wa miaka 29 akifunga mabao matatu kwenye mechi 17.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live