Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rais CAF ateta na Waziri Mkuu Dodoma

Waziri Mkuu Pic Data Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (kulia) akiwa na Patrice Motsepe ambae ni Rais wa CAF

Fri, 13 Aug 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Waziri Mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa leo asubuhi amekutana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF), Patrice Motsepe huko Dodoma kujadiliana na masuala kadhaa ya maendeleo ya mpira wa miguu.

Taarifa iliyotolewa na CAF, kikao hicho kimefanyika muda mfupi baada ya Motsepe kuwasili leo nchini ikiwa ni mara yake ya kwanza tangu alipochaguliwa kuwa Rais wa shirikisho hilo, Machi mwaka huu.

"Rais wa CAF pamoja na Waziri Mkuu wa Tanzania kwa pamoja watazungumza kuhusu mpira wa Miguu Tanzania, katika ukanda wa CECAFA na barani Afrika.

Watajadiliana pia kuhusu mashindano ya mashule ya CAF Pan African ambayo bado hayajazinduliwa. Dk. Motsepe alitangaza mwezi Aprili huko Kinshasa" ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa Motsepe atahudhuria mkutano mkuu wa CECAFA unaofanyika Dar es Salaam katika Hoteli ya Golden Tulip.

Rais Motsepe amepokelewa na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Innocent Bashungwa, Naibu Katibu Mkuu, Dkt. Ally Possi na Rais wa TFF, Wallace Karia.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz