Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raia wamjia juu Ronaldo, wadai malipo

Ronaldo Uso Kwa Usooo Raia wamjia juu Ronaldo, wadai malipo

Wed, 29 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Michael Sizemore, Mikey Vongdara na Gordon Lewis ambao ni raia kutoka nchini Marekani wamefungua kesi dhidi ya mchezaji wa Al Nassr Cristiano Ronaldo katika Mahakama ya Wilaya huko Florida wakimtuhumu kwa kutangaza biashara ya ubadilishanaji wa sarafu ya Kidijitali (Crypto Exchange Binance).

Ronaldo anadaiwa kutangaza dhamana ambazo hazijasajiliwa na kujihusisha na udanganyifu kikamilifu kwa kushirikiana na kampuni hiyo ya Binance.

Walalamikaji, wamesema wamepata hasara kutokana na uhamasishaji wa Ronaldo na wanataka kulipwa fidia ya kiasi kinachozidi dola Bilioni 1 sawa na TZS Trilioni 2.5, wakidai hasara za fedha kutokana na kutangaza kwake ubadilishanaji wa Crypto ambao sasa una matatizo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live