Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raheem Sterling kurejea kambini England

Raheem Strling Return Winga wa England, Raheem Sterling

Thu, 8 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa England Raheem Sterling anatarajiwa kurejea kwenye Kambi ya timu ya Taifa England baada ya kuhakikisha usalama wa familia yake kufuatia uvamizi nyumbani kwake London.

Chama cha Soka cha England FA, kimethibitisha kuwa nyota huyo atarejea kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa hatua ya robo Fainali dhidi ya Ufaransa siku ya Jumamosi.

Sterling aliondoka kwenye kambi ya timu ya England baada ya wezi kuvamia nyumba yake hali iliyotishia usalama wa familia yake.

Wezi hao wezi walichukua vito vya thamani vyenye thamani ya pauni 300,000 sawa na takribani TSH milioni 852.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live