Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Raha ya AJ hadi ampige Usyk, Fury

Usyk X AJ Raha ya AJ hadi ampige Usyk, Fury

Tue, 20 Aug 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati bondia Anthony Joshua akiwa na takribani mwezi mmoja kabla ya kupanda ulingoni kuzichapa na Daniel Dubois, bondia huyo bado hana amani moyoni hadi atakapompiga mmojawapo kati ya Oleksandr Usyk na Tyson Fury.

Akiwa tayari ameshapigana mara mbili na Usyk na mara zote kushindwa kwa pointi za majaji, Joshua 'AJ' anaelezwa kutokuridhika na kilichomtokea ndio sababu anaombea siku ziende haraka ili akutane na mmojawapo ili amtandike na dunia imtambue kama mbabe wa uzito wa juu duniani (heavyweight).

Hilo limefichukuliwa na promota mwenza wa Eddie Hearn katika kampuni ya Matchroom, Barry Hearn ambaye alidai bondia huyo hatulii mara zote anataka zaidi kupigana dhidi ya mshindi wa Usyk na Tyson ili amshinde na ndipo nafsi yake itatulia.

Chanzo: Mwanaspoti