Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rage awatabiria Yanga kutoboa makundi CAF

Mayele Na Mashabiki Yanga Rage awatabiria Yanga kutoboa makundi CAF

Thu, 6 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Zamani wa Simba SC Alhaji Ismail Aden Rage anaamini Yanga SC itafanya Vizuri kwenye Michezo yake miwili dhidi ya Al Hilal kwenye Caf Champions League na hatimaye kutinga kwenye makundi ya CAF CHAMPIONS LEAGUE.

Aden Rage anasema Imani hiyo inamjia kutokana na Ubora wa Kikosi cha Yanga SC kwenye hii misimu miwili, Benchi lao la Ufundi pamoja na Umakini walionao Viongozi kuelekea kwenye mashindano haya makubwa katika Bara la Afrika.

Aden Rage amesema;" Naiona Yanga SC ikifanya vizuri kwenye mashindano ya Kimataifa, wana Kikosi kizuri na wamejipanga, mimi naamini Yanga SC inatinga makundi ya CAF Champions League kwa kumtoa Al Hilal na sio kwa Yanga SC pekee hata Azam FC nawaona Makundi Kombe la shirikisho.

Ismail Aden Rage pia amewapa nafasi Azam FC ya kufanya vizuri anaamini na wao wamejipanga na wameimarika pia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live