Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rage aimwagia sifa lukuki Yanga

1c609d421a135cb5f4b9029bd4025d24.png Rage aimwagia sifa lukuki Yanga

Thu, 21 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MWENYEKITI wa zamani wa Simba, Ismail Rage amesema Yanga inayoonekana hivi leo ndio ile aliyoitaka Rais wa Awamu ya Tatu, Jakaya Kikwete.

Kikwete ambaye ni mpenzi wa Yanga aliwahi kuieleza klabu hiyo kuwa anawataka ichangamke wasiwe watu wa kulalamika, washindane na watani zao wa jadi Simba.

Akizungumza na gazeti hili juzi, Rage alisema Yanga imeanza kuleta changamoto na kuonesha ni namna gani wamechangamka msimu huu kutokana na ubora wao ikilinganishwa na misimu iliyopita.

“Yanga iko vizuri na imeonesha changamoto ya hali ya juu ila hata Simba bado ni wa moto wote ushindani umekuwa mzuri sana na kila mmoja ana nafasi ya kugombea taji la ligi,” alisema.

Kuhusu nafasi waiiyopo Yanga katika msimamo wa ligi kama itaweza kumudu kwa muda mrefu hadi ubingwa, Rage alisema ana amini kwa moto inayokuja nao Simba huenda ikarudi katika uongozi na hata kutetea taji.

Yanga ndio kinara ikiongoza kwa pointi 44 katika michezo 18 iliyocheza ikiwa na tofauti ya pointi tisa na Simba inayoshika nafasi ya pili kwa pointi 35 katika michezo 15 huku ikiwa nyuma kwa michezo mitatu.

Iwapo Simba itashinda michezo hiyo mitatu ya viporo na Yanga kusuasua itaifikia na pengine kuishusha kutoka kileleni kama kasi yake ya kufunga mabao mengi itaendelea.

“Simba itafika tu mdogo mdogo kwa sasa tumeawaachia kwanza watani zetu waongoze na muda sio mrefu tutarejea kileleni,” alisema.

Hata hivyo, alisema licha ya kuwa Simba inaonekana ya moto hata Yanga sio ya kubezwa msimu huu inaweza kufanya mapinduzi.

Chanzo: habarileo.co.tz