Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rage: Simba, Yanga wakutane Fainali ya CAFCL

Simba Yanga WA0007 Rage: Simba, Yanga wakutane Fainali ya CAFCL

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa zamani wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amesema kuwa mashabiki wanapaswa kuzipa sapoti timu zao za nyumbani Simba na Yanga na wala si kukasirika endapo timu moja inapofanya vizuri kwenye michuano.

Rage amesema hayo kufuatia matokeo mazuri waliyopata Yanga juzi, Februari 24, 2024 kwa kuifunga CR Belouizdad bao 4-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya CAFCL wakiwa na mchezo mmoja mkononi, na kuvunja rekodi yao ya miaka zaidi ya 52 iliyopita kufika hatua hiyo.

“Sio Yanga pekee, hata Simba nao wanacheza vizuri, wanapambana, wametoa sare ugenini na wana mechi muhimu ya mwisho, tuhakikishe timu hizi mbili zinaingia zote robo fainali, ni heshima kwa nchi yetu.

“Timu za Afrika zimeshaanza kuziogopa Simba na Yanga, kwa hiyo tuache ushabiki wa kizamani kwamba kwa vile mimi ni Simba kwa hiyo Yanga wakifanya vizuri unakasirika, au wewe ni Yanga halafu Simba akifanya vizuri unakasirika, huo ni ujinga tu wala sio ushabiki.

“Mimi nasema tuhakikishe timu zetu zikiingia huenda wakakutana nusu fainali au fainali na ikawa raha tupu,” amesema mzee Rage.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live