Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rage: Bao 5-1, Yanga hawajavunja rekodi ya kuifunga Simba

Rage 0001 Mzee Ismail Rage.

Thu, 9 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage amesema kuwa, watani zao ambao ni Yanga bado hawajavunja rekodi ya kipigo kizito walichopewa na Simba mwaka 2012.

Rage amesema hayo kufuatia timu yake kupokea kichapo cha bao 5-1 kutoka kwa watani zao Yanga, Jumapili iliyopita katika Dimba la Mkapa huku akidai kuwa kipigo vya Simba kufungwa goli 5-1 na Yanga bado hakifikii kile cha Yanga kufungwa na Simba goli 5-0

"Yanga bado hawajalipa deni letu, wao walitufunga bao 5 mwaka 68, sisi tukaja kulipa tukawapiga 6-0, bado wakawa wanaongea ongea tukawapiga 5-0, sasa wao wametufunga 5-1 bado hawajalipa deni letu," amesema Mzee Rage.

Nini maoni yako?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live