Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Rafael Leao achukia mpira kisa takwimu

Rafael Leao Stats Rafael Leao

Wed, 20 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Juzi juzi hapa Rafael Leao alisema mpira wa sasa umeaharibika kutokana na mtazamo unaoamini takwimu ndio kitu kinachompima mchezaji.

Sasa hivi mtu atakwambia fulani sio mkali sababu hana takwimu kubwa kihivyo. Lakini kiuhalisia ukiangalia unakuta mchezaji huyo anafanya kazi kubwa sana kuhakikisha timu inapata matokeo.

Pengine anatengeneza nafasi nyingi lakini zinatumiwa kidogo, pengine yeye anaichezesha timu kwa asilimia kubwa kuliko kuhusika kwenye mabao (kama alivyokuwa Eden Hazard kipindi kile).

Rafael Leao yeye amesema anapenda kuwa mburudishaji zaidi kuliko kukimbilia takwimu.

Na kweli Rafael Leao ni joy kumtazama, enjoyment unayoipata ukimwangalia Rafael inakutosha na hata huhitaji hayo mengine.

Ndio maana zamani entertainers walikuwa wanapendwa zaidi kuliko ambao wapo juu kitakwimu.

Kama ukifanikiwa kutoboa kote kwenye takwimu na entertainment basi ni vizuri zaidi, mfano Neymar, Ronaldo de Lima nimeona kitakwimu na kiburudani waliweza vyote.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live