Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RS Berkane wamshtaki refa Ndala CAF, Wadai alihongwa na Simba

Jacques Ndala Chuma Jacques Ndala Chuma

Mon, 14 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya RS Berkane ya Morocco imewasilisha malalamiko kwa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) kuhusu mwamuzi wa DR Congo, Jacques Ndala Chuma alichezesha mchezo dhidi ya Simba SC na kutaka afungiwe.

Berkane wanadai Ndala alihongwa ndio maana aliwanyima penati kwenye mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Pia, wanasema walipata bao la wazi lakini walinyima kwa sababu kwa sababu mchezaji wao alikuwa tayari ameshaotea (offside). Wamorocco hao walisema, Simba ilipoteza muda mwingi na mwamuzi wa akiba akaongeza dakika nne tu za kuchezwa.

Klabu hiyo inaitaka CAF kumuadhibu mwamuzi na wasaidizi wake wote kwa kufungiwa ikiwezekana kwa kushindwa kutenda haki katika mchezo huo uliomalizika kwa Simba kuibuka na ushindi wa bao 1-0.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live