Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

RS Berkane wagomea mechi na USM Alger, wasepa kwao

Berkane YAEsbiQ RS Berkane wagomea mechi na USM Alger, wasepa kwao

Sun, 21 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Utata umegubi ka kwenye pambano la RS Berkane dhidi ya USM Algiers ambapo nusu fainali hiyo ya shirikisho Afrika imeshindwa kupigwa jijini Algiers nchini Algeria kutokana na kuwa Berkane wana jezi zenye ramani kamili ya nchi ya Morocco ikiwemo eneo la Western Sahara, hii ikiwa tofauti na siasa ya Algeria ambapo wao wapo upande wa uhuru wa Western Sahara kutoka kwa Morocco.

Algeria wanawapa nguvu kundi maarufu la Polisario Front separatist movement, ambapo agenda yao ni Western Sahara iwe huru! Kutokana na hilo Berkane walizuiwa Airport kwa muda mrefu na waliswali swala ya ljumaa hapo na walifanya mazoezi mepesi, baadae waliruhusiwa kuondoka ila jezi zilizuiwa kutoka ikitajwa Berkane wacheze mechi bila ramani ya Morocco kwenye jezi.

Kutokana na sakata hilo shirikisho la soka la Morocco limetuma ndege binafsi kuwachukua Berkane na kurudi nyumbani kwakuwa mzigo wa jezi imeshindikana kuzitumia, mechi imeghairishwa rasmi tukisubiri maamuzi kutoka CAF.

Kidiplomasia Algeria na Morocco hawapo sawa tangu zamani ikumbukwe Sand War ya 1963, Western Sahara War of 1975-1991 na walishawahi kufungiana mipaka mwaka 1994, kifupi sana hili suala la Sahrawi ni jambo zito sana na sio suala la mpira tena bali diplomasia, Algeria akitajwa ni chanzo kikuu cha mgogoro huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live