Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

REMONTADA yawapa jeuri Azam FC

Azam FC . REMONTADA yawapa jeuri Azam FC

Fri, 14 Oct 2022 Chanzo: Eatv

Azam inaendelea kujifua kwenye Uwanja wa Azam Complex ikijiandaa na mechi hiyo ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku Kocha Lavagne akitamba anaamini vijana wake watapindua meza licha ya aibu waliyiopata ugenini.

Ushindi wa mabao 4-0 ndio utaifanya Azam iiondoshe Akhdar na kusonga mbele na kikosi kizima chini ya Kocha Lavagne wanaamini inawezekana na wameweka mipango mikakati ya kupindua meza hiyo kibabe.

“Hadi sasa bado tunajitafuta, hatujawa na kikosi cha kwanza cha kudumu lakini tuna aina ya kila mchezaji. Kila mchezo unakuwa na mbinu zake, mchezo wa nyumbani tunahitaji kushambulia na kutafuta mabao zaidi kwahiyo tutabadilika karibu kila eneo tofauti na tulivyoicheza ugenini,” amesema Lavagne .

Kwa upande wa wachezaji, beki wa kikosi hicho, Nathanael Chilambo ameeleza wanaendelea kujifua ili kuhakikisha wanakuwa bora na kufanya vizuri mechi ijayo.

“Matokeo ya kwanza yalituumiza lakini imetupa funzo na tunajiandaa ili kuwa bora katika mechi ya marudiano,” amesema Chilambo.

 

Chanzo: Eatv