Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

REMONTADA: Azam vs Al Akhdar kiingilio jezi

Azam FC Muda Bado REMONTADA: Azam vs Al Akhdar kiingilio jezi

Sat, 15 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Azam FC imetanganza kuwa mchezo wao wa marudiano wa Kombe la Shirikisho barani Afrika dhidi ya Al Akhdar ya Libya hautakuwa na kiingilio, zaidi ya mashabiki kuvaa jezi ya Azam ya aina yoyote ili kuingia uwanjani.

Mchezo huo utapigwa kesho Jumapili, Oktoba 16 kwenye uwanja Azam Complex, Chamazi kuanzia Saa 1:00 Usiku.

Kupitia kwenye kurasa zao za mitandao ya kijamiii Azam FC wameandika "Vaa jezi yako yoyote ya msimu wowote ya Azam FC, halafu tukutane Azam Complex tukapindue meza kibabe"

Azam wanaingia kwenye mchezo huo wakiwa na slogan ya "REMONTADA Inawezekana!" kwa lengo la kupindua matokeo ya mechi ya kwanza iliyochezwa Libya kwa Azam FC kufungwa mabao 3-0.

"REMONTADA Inawezekana" Kila la kheri Wawakilishi pekee wa Tanzania kwenye Kombe la Shirikisho barani Afrika.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live