Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

REKODI: Huyu ndio mchezaji aliecheza dakika nyingi bila kugusa mpira Uwanjani

Thomas Sweswe Thomas Sweswe

Mon, 11 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Thomas Sweswe (42) ndiye mchezaji anayeshikilia rekodi ya kucheza dakika 90' bila kuugusa mpira Uwanjani.

Hii ni miongoni mwa rekodi za kushangaza na kuchekesha Duniani kwenye soka iliyowekwa na mchezaji raia wa Zimbabwe Thomas Aaron Langu Sweswe (2009).

Thomas Sweswe alizaliwa Nchini Zimbabwe mwaka 1981,

Mwaka 2002 alianza rasmi maisha yake ya soka la kulipwa huko nchini kwao Zimbabwe akicheza katika nafasi ya beki wa kati,

Sweswe alifanikiwa kucheza timu saba (7) tofauti Kwenye nchi mbili, Africa kusini na Zimbabwe,

Msimu wa mwaka 2009/2010 akiwa na club yake ya Kaizer chiefs iliweka rekodi hiyo baada ya kucheza mpira kwa dakika 90' bila kuugusa mpira, Baada ya mechi aliulizwa iliwezekana vipi kucheza kwa dakika (90') bila kugusa mpira ? akasema,

Kutokana na tukio hilo la kushangaza Sweswe akapewa tuzo ya mchezaji bora wa mchezo yaani Man of the match,

MWAMBA AKATUNDIKA DALUGA RASMI

2016 Thomas Sweswe alistaafu soka kutoka na majeraha (27 March 2017), beki huyo alichaguliwa kuwa Katibu mkuu wa Shirikisho la soka Zimbabwe.

Hii ni kutokana na kuitumikia vyema nchi yake kwenye mpira wa miguu na uzalendo aliokuwa nao kwa nchi yake ya Zimbabwe.

Rekodi hii inatambulika na jarida kubwa la kutunza rekodi Duniani liitwalo kwa jina la 'GUINNESS BOOK OF RECORDS'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live